Miongozo ya ZanFix

Tunathamini uwazi. Tafadhali pitia miongozo na taratibu zetu kabla ya kujiunga na ZanFix.

Iliyosasishwa Tarehe: 23 Aprili, 2026

Utangulizi

ZanFix ni jukwaa la kisasa la mtandaoni linalotumika kama orodha ya biashara (Business Directory) kuwaunganisha wauzaji, watoa huduma, na wateja ndani ya Zanzibar. ZanFix inafanya kazi kama daraja la mawasiliano pekee na haihusiki na mchakato wa mauzo, malipo, au usafirishaji wa bidhaa/huduma.

Kwa kujiunga na ZanFix, unakubali kufuata Miongozo na Taratibu hizi kwa ukamilifu.

Ufafanuzi wa Istilahi

  • ZanFix - Jukwaa la mtandaoni linalomilikiwa na ZanFix linalotoa huduma ya kuunganisha na kutangaza wafanyabiashara.
  • Mfanyabiashara - Mtu binafsi au kampuni inayojitangaza kupitia ZanFix ili kupatikana na wateja.
  • Mteja / Customer - Mtu anayetafuta bidhaa au huduma kupitia ZanFix.
  • Bidhaa / Products - Vitu vinavyouzwa na mfanyabiashara kupitia jukwaa letu.
  • Huduma / Services - Kazi au utaalamu unaotolewa na mtoa huduma kwa malipo.
  • Taarifa za Kibinafsi - Data yoyote inayoweza kukutambulisha kama jina, namba ya simu, anuani, barua pepe, n.k.
  • Muamala (Transaction) - Makubaliano yoyote ya kibiashara au kifedha yanayofanyika moja kwa moja kati ya Mfanyabiashara na Mteja nje ya jukwaa la ZanFix.

Kujiunga na ZanFix.

1. Masharti ya Kujiunga

  • (Mfanyabiashara) Kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi
  • Kuwa na biashara halali iliyosajiliwa (au utaratibu wa kufanya biashara)
  • Kutoa taarifa sahihi na za kweli kwenye fomu ya usajili
  • Kukubali sheria, kanuni na sera za faragha za ZanFix
  • Kukubali kuwa ZanFix ni jukwaa la matangazo na si msimamizi wa mauzo yako.

2. Mchakato wa Kujiunga

  • Jaza fomu ya usajili kwa taarifa kamili na sahihi
  • Wasilisha maombi yako kwa timu ya ZanFix
  • ZanFix itachambua maombi yako ndani ya masaa 24 ya kazi
  • Utapokea taarifa ya kukubaliwa au kukataliwa kupitia barua pepe au WhatsApp
Kumbuka: ZanFix ina haki ya kukataa ombi lako bila kutoa sababu ikiwa sheria au kanuni hazijatimizwa.

Majukumu ya Mfanyabiashara

  • Ukweli na Uaminifu - Kutoa maelezo sahihi kuhusu bidhaa au huduma zako.
  • Miamala ya Kifedha - Mfanyabiashara anawajibika kikamilifu kukubaliana na mteja kuhusu namna ya malipo na kutoa risiti halali kwa mujibu wa sheria.
  • Usalama - Kuchukua tahadhari wakati wa kukutana au kufanya biashara na wateja wapya wanaopata mawasiliano yako kupitia jukwaa.
  • Bei Sahihi - Kuweka bei zilizo wazi na bila siri.
  • Kutunza Siri za Jukwaa - Kutoshirikisha taarifa za ndani za ZanFix na watu wengine.
  • Kufuata Sheria za Nchi - Kuzingatia sheria za Zanzibar na Tanzania kuhusu biashara, ushuru na ulinzi wa watumiaji.
  • Kulipa Ada Zilizokubaliwa - Kukamilisha malipo yoyote yanayotakiwa na ZanFix kwa wakati.

Bidhaa na Huduma Zisizoruhusiwa

ZanFix haito orodhesha bidhaa au huduma zifuatazo:

  • Bidhaa haramu au zilizopigwa marufuku na sheria
  • Dawa za kulevya au vitu vya kusisimua
  • Silaha au vitu vya hatari
  • Bidhaa ghushi au zilizoivunja hakimiliki
  • Huduma za kashfa au ulaghai
  • Maudhui ya chuki, ubaguzi au unyanyasaji
  • Bidhaa au huduma zinazokiuka maadili ya jumuiya

Malipo na Ada

ZanFix haishiriki, haipokei, wala haisimamii malipo yoyote ya bidhaa au huduma kati ya mteja na mfanyabiashara.

  • Ada ya Usajili - Hakuna ada ya usajili wa awali. Kujiunga ni bure!
  • Ada ya Matangazo (Subscription) -ZanFix inaweza kutoza ada ya kudumu (fixed fee) kwa ajili ya kuorodhesha biashara au kuipa kipaumbele kwenye matokeo ya utafutaji.
  • Miamala ya Nje - Malipo yote yatafanyika moja kwa moja kati ya mteja na mfanyabiashara (kwa taslimu, benki, au simu). ZanFix haitahusika na madai ya marejesho ya fedha au migogoro ya malipo.

Kusitisha Ushirikiano

ZanFix inaweza kusitisha ushirikiano wako kwa sababu zifuatazo:

  • Ukiukaji wa sheria au kanuni zozote za ZanFix
  • Kutoa taarifa za uongo au kughushi hati
  • Kushindwa kutoa huduma au bidhaa kwa wateja
  • Madai mengi ya wateja dhidi yako

Wewe unaweza kusitisha ushirikiano kwa:

  • Kuwasilisha ombi la kuondoka kwa maandishi
  • Kutoa taarifa ya siku 7 kabla ya kuondoka

Mchakato wa Uhakiki (Verification Process)

ZanFix imejitolea kuhakikisha kuwa jukwaa letu linatumiwa na wafanyabiashara waaminifu na halali. Kabla ya biashara yako kuanza kuonekana hadharani, timu yetu itafanya ukaguzi ufuatao:

01

Uhakiki wa Nyaraka

Kukagua leseni ya biashara, kitambulisho cha taifa (NIDA), au vibali husika vya mamlaka za Zanzibar (kama ZRB, ZIPA, au Bodi ya Utalii kwa huduma za kitalii).

Leseni ya Biashara Kitambulisho cha NIDA Vibali vya ZRB/ZIPA Bodi ya Utalii (kwa huduma za kitalii)
02

Uthibitisho wa Mawasiliano

Kupiga simu au kutuma ujumbe kwenye namba zilizotolewa ili kuhakikisha kuwa mmiliki wa biashara anapatikana na anajibu kwa wakati.

Tutawasiliana nanyi kwa namba mtakayotowa kwenye fomu ya usajili. Hakikisha namba yako ni sahihi na inapatikana.
03

Ukaguzi wa Eneo (Physical Verification)

Kwa biashara zenye ofisi au maduka ya kudumu, timu ya ZanFix inaweza kuhitaji picha za eneo la biashara au kutembelea eneo hilo ili kuthibitisha uwepo wake.

Tayarisha picha za duka lako, leseni iliyowekwa ukutani, na eneo la jirani kwa uthibitisho wa haraka.

Kumbuka Muhimu

ZanFix ina haki ya kuomba maelezo ya ziada wakati wowote au kuiondoa biashara kwenye jukwaa ikiwa itagundulika kuwa taarifa za uhakiki zilikuwa za uongo au biashara imepoteza sifa za kisheria.

Muda wa Kukamilisha Uhakiki

Siku 1-2 Uhakiki wa Nyaraka
Siku 1-2 Uthibitisho wa Mawasiliano
Siku 2-3 Ukaguzi wa Eneo (kama unahitajika)
Jumla ya muda: Siku 2 hadi 7 za kazi (kwa wastani)

Sera ya Faragha (Privacy Policy)

ZanFix inathamini faragha yako na inajitolea kulinda taarifa zako za kibinafsi. Sera hii inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa zako.

1. Taarifa Tunazokusanya

  • Jina kamili
  • Namba ya simu
  • Anuani / Eneo la biashara
  • Jina la biashara / duka

2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

  • Kukuhudumia - Kutengeneza na kusimamia akaunti yako
  • Mawasiliano - Kuonyesha mawasiliano yako kwa wateja wanaohitaji huduma zako.
  • Kuboresha jukwaa - Kuchambua takwimu na kuboresha huduma zetu

3. Usalama wa Taarifa Zako

ZanFix inatumia teknolojia za kisasa za usalama (encryption, firewalls, access controls) kulinda taarifa zako dhidi ya upotevu, wizi au matumizi mabaya. Taarifa zako zinahifadhiwa kwenye seva salama na wahitimu wetu wanaofuzu ndio pekee wenye ufikiaji.

Uthibitisho wa Usalama: Seva zetu zinalindwa na SSL encryption (TLS 1.3), firewall, na kaguzi za usalama mara kwa mara.

4. Kushiriki Taarifa na Watu wa Tatu (Third person)

ZanFix HAIUZI au HAISHIRIKI taarifa zako za kibinafsi kwa watu wa tatu kwa madhumuni ya kibiashara. Hata hivyo, tunaweza kushiriki taarifa zako katika mazingira yafuatayo:

  • Kwa mamlaka za sheria ikiwa tunatakiwa kwa sheria
  • Kwa kukusanya takwimu za jumla zisizokutambulisha wewe

5. Haki Zako kuhusu Taarifa Zako

Kwa mujibu wa sheria ya ulinzi wa data, una haki zifuatazo:

  • Kujua - Kujua taarifa gani tunazokuwa nazo
  • Kusahihisha - Kuomba taarifa zako zisizosahihi zirekebishwe
  • Kufuta - Kuomba taarifa zako zifutwe (ikiwa hakuna sababu ya kisheria ya kuzihifadhi)
  • Kukataa - Kukataa tunapotumia taarifa zako kwa madhumuni ya uuzaji

Ili kutumia haki zako, wasiliana nasi kwa: +255 651 527 779

6. Mabadiliko ya Sera ya Faragha

Tunaweza kusasisha Sera ya Faragha mara kwa mara. Mabadiliko yoyote muhimu tutakujulisha kwa barua pepe au kwa taarifa kwenye jukwaa letu. Sera ya sasa inakuwa halali mara tu inapochapishwa hapa.

Taarifa Zetu za Mawasiliano

ZanFix (Main Office)
Fuoni, Zanzibar, Tanzania
+255 651 527 779
infozanfix@gmail.com
+255 651 527 779 (WhatsApp Support)

Kukubali Sheria na Kanuni

Kwa kujiunga na ZanFix, unathibitisha kuwa umeisoma, kuelewa na kukubali sheria, kanuni na sera za faragha zilizoelezwa hapo juu. Unakubali kufuatwa na mabadiliko yoyote ya baadaye ambayo yanatolewa na ZanFix.

Kukubali kwako:

"Nimesoma, nimeelewa na nakubali sheria, kanuni na sera ya faragha ya ZanFix kwa hiari yangu."